Salamba amesema mashabiki wanapaswa waelewe kwamba kazi yake ni mpira na anafanya jitihada kubwa kila siku kulinda ubora wake.
"Mpira una wakati unakukubali na muda mwingine unashindwa kukukubali hiyo haimaanishi umeshindwa kuonyesha uwezo ila muda ukifika kila kitu kitakuwa sawa na jitihada zangu zitakuwa wazi kwa mashabiki wangu," alisema Salamba.
Salamba ana mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara, katika mashindano ya Mapinduzi alicheza michezo mitano hakufanikiwa kufunga bao.
Kwa yule Salamba wa Mapinduzi cup basi wakati wowote atatolewa kwa mkopo pale Simba yaani inasikitisha hawa vijana wetu sijui namna gani baada yakwenda Simba kuongeza kiwango kwakuwa wana karibu kila kitu mchezaji anachokihitaji kujiendeleza,mshahara kwa wakati, kocha bora, hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki lakini la kushangaza vijana wetu wanafikia kubweteka yaani bure kabisa.
ReplyDeleteKwa kweli Salamba nilikuwa namkubali sana, na ikafikia wakati Kocha alipokuwa anamuweka benchi na kumuingiza dakika za mwisho nilikuwa namlaumu sana kocha. Lakini kwa kiwango alichokionyesha Salamba kwenye kombe la Mapinduzi! Nakubaliana na Kocha, maana Salamba amepewa nafasi kwa dakika zote 90 kwa mechi alizopangwa, lakini ameshindwa kutushawishi, na mimi binafsi sikuona alichokifanya, kwasababu alikuwa anazunguka tu uwanjani, hakabi, akipata mpira anapoteza pasi, akiingia ndani ya 18 anabutua tu hovyo hata kama yupo nafasi ya kutoa pasi ya mwisho ya goli, anataka yeye ndo apige tu!, yaani hakuna kitu kabisa!. Anajikaribisha mwenyewe kwenye benchi, hakuna juhudi yoyote ile anayoionyesha! Kwa aina ile ya uchezaji ndo anataka kwenda Ubelgiji! labda kwenye timu za shule za msingi ila sio timu za ligi.
ReplyDeleteSawa kabisa
Delete