KOCHA Mkuu wa Mwadui FC, Ally Bizimungu amesema anatambua ubora wa kikosi cha Yanga ila amejipanga kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wake wa kwanza nyumbani.
Mwadui leo watakuwa Uwanja wa Taifa wakimenyana na Yanga huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa mzunguko wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-1.
Bizimungu amesema amewapa mbinu mpya wachezaji wake ambazo zitawasaidia kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao licha ya kuwa watakuwa ugenini.
"walifanikiwa kupata matokeo nyumbani kwetu nasi tuna nafasi ya kupata matokeo kwao, hatuna wasiwasi katika hilo kila kitu kinawezekana na morali ya wachezaji ni kubwa," alisema Bizimungu.
0 COMMENTS:
Post a Comment