MCHEZO ULIOIHUSISHA SIMBA WAPIGWA KALENDA, UTAPANGIWA TAREHE NYINGINE
Mchezo kati ya Mabingwa watetezi Simba na Lipuli ambao ulipaswa uchezwe kesho umepelekwa mbele na Bodi ya Ligi Kuu Bara mpaka pale utakapopangwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuna ugumu wa kupanga ratiba kutokana na timu kushiriki michuano mbalimbali.
"Kwa sasa viporo vya Simba vitapangiwa tarehe wanaweza kucheza mchezo mmoja ama miwili mwezi huu wa Kwanza Ila mwezi wa pili watakamilisha michezo yao Kwa asilimia kubwa," alisema Wambura.
Hivi sasa kikosi cha Simba kipo kwenye maandalizi ya kucheza na As Vita ya Congo ambapo mechi itachezwa Jumamosi ya wiki hii ugenini.
Tayari Kocha Patrick Aussems ameshaanza kuwanoa wachezaji wake kwa mazoezi ya kufa mtu ikiwa ni mapema baada ya kumaliza kazi kwa waarabu, JS Saoura waliolala kwa mabao 3-0 Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment