KAZI IPO, KIGOGO YANGA AIITA SERIKALI IFANYE UCHUNGUZI MKALI KLABUNI
Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti katika klabu ya Yanga, Mbaraka Igangula ameitaka serikali kuweka mkono wake katika uchaguzi ambaoulipaswa kufanyika Januari 13 2018.
Maamuzi hayo amekuja nayo mara baada baadhi ya wanachama kusababisha mahakama izuie uchaguzi huo baada ya kufungua kesi wakidai kuna sintofahamu imejitokeza.
Igangula amefunguka kuitaka serikali iingilie kati akiamini kuna baadhi ya watu wamefanya maamuzi hayo kwa sababu zao binafsi.
Ameongeza kuwa Yanga imekuwa na makundi mawili ambapo moja alieleza linataka uchaguzi ufanyike na lingine likipinga usifanyike.
Kitendo hicho kimemkera Igangula ambaye anahitaji serikali ijaribu kuchunguza suala hilo pengine inawezekana kuna namna imefanyika.
Mahaka ilizuia uchaguzi wa Yanga ambapo sasa utapangiwa tarehe nyingine endapo mahakama itafikia maamuzi ya kuuruhusu ufanyike.
Serikali ni mimi, wewe, mahakama sasa unataka serikali gani weke mkono wakati mahakama imeshazuia? Acha vyombo vya dola vifanye kazi kwa wanaotaka haki yao...
ReplyDelete