January 19, 2019



UONGOZI wa Azam FC umepania kubeba pointi tatu mbele ya wapinzani wao Mwadui FC katika mchezo utakaochezwa leo Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema anatambua ubora wa kikosi cha Mwadui ila wana imani ya kutumia vema Uwanja wao wa nyumbani leo kupata matokeo.

"Wapinzani wetu tunawatambua ni bora na wana kikosi chenye ushindani ila ni wakati wetu kutumia Uwanja wa nyumbani kupata matokeo,tunakumbuka mzunguko wa kwanza tulipata sare kwao sasa hapa kazi ni moja tu pointi tatu tunahitaji," alisema Maganga.

Azam na Mwadui wamekutana mara saba kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara na katika michezo hiyo Azam wamefanikiwa kushinda mara tano na wametoa sare mara mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic