BILIONEA ASUKA MCHONGO WA USHINDI YANGA
Aisee!! Yanga kweli inapendwa, kwani wachezaji walihakikishiwa kulamba mkwanja mrefu na kupewa malazi ya kiwango cha juu kama wataifunga Stand United, jana Jumamosi kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. Yanga imekuwa na msimu mzuri ambapo mpaka jana kwani mpaka jana ilikuwa haijapoteza mchezo wowote wa ligi kati ya michezo 20.
Stand wao katika mechi 21 wameshinda sita, sare nne na kupoteza 11 hivyo wapo nafasi ya 16. Sasa juzi Alhamisi, Yanga ilisafiri kwa ndege kwenda Mwanza ambapo hapo walitulia na kupata chai baadaye wakasafiri hadi Shinyanga kwa basi kwa ajili ya mchezo huo.
Sasa baada ya kumaliza mechi hiyo leo watageuza kwa basi kwenda Mwanza ambapo hapo wangekutana na shangwe kubwa kama wangeshinda mchezo huo.
Katibu Mkuu wa Matawi ya Yanga, Mhando Madega alisema kuwa, kabla Yanga haijatua jijini Mwanza tayari alishapewa maagizo mapema tu na bilionea maarufu
jijini hapa ambaye ni Yanga ‘lialia’, Yanga Makaga, kwamba ahakikishe wachezaji na msafara mzima unapokewa kifalme.
Aliongeza kuwa Makaga alisema baada ya Yanga kurejea kesho yake yaani Jumapili kutokea Shinyanga itafikia Hoteli ya Pigeon iliyopo jijini hapa ambapo watapata chakula cha mchana na baadaye wataondoka kwa ndege kurejea jijini Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata.
Madega aliongeza kuwa, Makaga anafanya hivyo kwa kuwa pia kutakuwa na bonasi nzuri kwa wachezaji wote ambayo naamini kila mmoja ataifurahia na kwamba anafanya hivyo ili kuifanya Yanga ishinde mechi zake za Kanda ya Ziwa.
“Kuna maagizo nimepewa na mlezi wetu wa kanda, Yanga Makaga kwamba Yanga ikishinda kuna bonasi atatoa kwa wachezaji wetu kama motisha, hajaniambia ni kiasi gani lakini naamini kwamba wachezaji watafurahia kwa kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa Yanga inaposhinda kwa Kanda ya Ziwa.
“Mlezi wetu Makaga ambaye ndiye ameandaa kila kitu kwa ajili ya mapokezi ya Yanga ameniachia maagizo kuwa Yanga itawasili hapa Mwanza kuanzia saa tano asubuhi siku inayofuata baada ya mechi yetu na Stand
“Msafara wote utapumzika katika Hoteli ya Pigeon na kula chakula cha mchana na baadae timu itasafiri majira ya jioni kuelekea Dar kwa ndege, hivyo haya yote yamefanywa na Yanga Makaga ambaye amekuwa akijitoa kwa nguvu zote kuhakikisha Yanga inapata ushindi,” alisema Madega.
Ikumbukwe kuwa Makaga ambaye anamiliki vivuko vya kutoka Mwanza kwenda Sengerema na mabasi ya abiri amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Yanga inapata matokeo katika ukanda wa ziwa.
Zamani ilikuwa ngumu Yanga kupata ushindi ukanda huu lakini msimu huu wamevuna alama sita kutokana na kuwafunga Mwadui ya Shinyanga na Kagera Sugar ya Kagera, baada ya mechi hizo bilionea huyo aliwapa motisha wachezaji kisha akawasafirisha kwa ndege wachezaji na benchi la ufundi kwenda Kagera na Da
0 COMMENTS:
Post a Comment