January 14, 2019



OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema anatambua umuhimu wa kujitoa kwa jamii kutokana na namna ambavyo wanampa sapoti hali ambayo imemfanya awe kwenye mpango wa kuzindua kampuni.

Manara amesema kuwa mpango mkubwa ni kurejesha kwa jamii kile ambacho amekipata kwa jamii pamoja na kuwasaidia wenye mahitaji mbalimbali kupitia bidhaa mpya atakayoizindua januari 27.

"Januari 27 natarajia kuzindua perfume yangu ambayo itaitwa De la Boss kwa ajili ya watu wote, nataka kila mtanzania kuanzia rika ya chini mpaka ile ya juu awe na uwezo wa kuipata perfume yangu ambayo ina harufu ya tofauti.

"Katika hayo pia nina mpango wa kurejesha shukrani kwa jamii yangu kwa kuwa natambua kwamba mimi ni mlemavu hivyo nitaleta pia losheni maalumu kwa ajili ya walemavu wa ngozi ili ziweze kutumika, hivyo sapoti kubwa katika hili nahitaji," alisema Manara.

1 COMMENTS:

  1. Big up Haji Manara Mwenyezi Mungu atakubariki kwa kusaidia waja wake walio na ulemavu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic