January 14, 2019



WAKATI Simba wakichekelea ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura, hali imekuwa mbaya kwa wapinzani wao AS Vita mbele ya Al Ahly ya Misri kwa kukubali kichapo cha mabao 2-0.

Simba itakuwa kazini Januari 19 nchini Congo kucheza na AS Vita, mchezo wa kundi D ambalo Simba wapo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 Kocha wa Dodoma FC na mwanachama wa Simba, Jamhuri Kwihwelu 'Julio' amesema kwa namna Simba walivyoanza wananafasi ya kuwapiga AS Vita endapo hawatabweteka na ushindi wao.

"Wachezaji wa Simba wanapaswa watambue wana kazi nyingine ya kufanya ili kuendeleza furaha ya mashabiki na kufikia malengo ambayo wamejiwekea, mchezo wao ujao watakuwa ugenini ila tayari wapinzani wao wamechanganyikiwa kwa kichapo.

"Mabao 2 waliyofungwa yatawafanya waingie uwanjani wakiwa na presha, sasa hiyo itakuwa fursa kwa Simba kuitumia vizuri na kupata matokeo ugenini wakishindwa kushinda walazimishe sare ili wakija hapa nyumbani wachukue pointi tatu," alisema Julio.

AS Vita ni miongoi mwa timu ambayo ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Raja Casablanca na ilipoteza kwenye mchezo huo, itacheza na Simba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa jumamosi.

3 COMMENTS:

  1. Moja ya jambo Simba wanatakiwa kulitilia maanani sana ni kuwahi kwenda Congo mapema kwani ile nchi haipo sawa jambo la siku moja linaweza kuchukua siku mbili na kama jambo hilo litaingizwa na fitina za kimkakati kutoka kwa wenyeji na kama kawaida timu za kikongo kwa fitna kuliko hata za warabu, Simba ikichelewa kwenda Congo itajikuta katika wakati mgumu sana kitu kitakachopelekea kufanya vibaya kwenye mchezo huo.

    ReplyDelete
  2. Awa walifungwa na Raja Casablanca 3-0 fainal tena kwa mizengwe mchezo wa marudiano wakashinda 3-1 na mechi na Ahly waliofungwa 2-0 zengwe lilikuwa kubwa kutoka kwa marefa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic