HIKI NDICHO KIKOSI HATARI ZAIDI ULAYA
England walifika nusu fainali katika Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018, lakini hakuna mchezaji hata mmoja wa timu hiyo ya taifa aliyejumuishwa kwenye kikosi bora cha wachezaji 11 Ulaya, chaguo la mashabiki kwa mwaka huo.
Ingawa kuna wachezaji watatu wanaocheza Ligi ya Premia kwenye kikosi hicho, hata nahodha wa England Harry Kane aliyeshinda tuzo ya mfungaji bora zaidi Urusi, hajajumuishwa.
Kiungo wa Liverpool Virgil van Dijk na wachezaji wawili wa Chelsea N'Golo Kante na Eden Hazard wamo kwenye kikosi hicho cha wachezaji XI.
Cristiano Ronaldo ni miongoni mwao, ambapo amejumuishwa kwa mara ya 13 sasa, na kuwa mchezaji aliyejumuishwa mara nyingi zaidi.
Mshambuliaji huyo wa Ureno ambaye sasa huchezea Juventus ya Italia, aliisaidia klabu yake ya zamani Real Madrid kushinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya tatu mtawalia mjini Kiev, Ukraine mwezi Mei ambapo waliwalaza Liverpool.
Mchezaji mwenzake wa zamani Madrid, Luka Modric, ambaye alitamba sana akichezea Croatia na kuwasaidia kufika fainali Kombe la Dunia, ndiye mchezaji aliyepigiwa kura nyingi zaidi na mashabiki - kura 115,440.
Nyota wa Barcelona Lionel Messi amejumuishwa kwa mara ya kumi katika kikosi hicho.
Wageni wapya kwenye kikosi hicho ni mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe pamoja na Marc-Andre ter Stegen, Van Dijk, Raphael Varane, na Kante.
Image caption
Harry Kane alikuwa mfungaji bora Kombe la Dunia 2018
Kikosi hicho, ambacho kina wachezaji watano kutoka Real Madrid, kiliandaliwa kwa kutumia kura milioni mbili za mashabiki waliojisajili na Uefa.
Marc-Andre ter Stegen (FC Barcelona & Ujerumani)
Sergio Ramos (Real Madrid CF & Uhispania)
Virgil van Dijk (Liverpool FC & Uholanzi)
Raphael Varane (Real Madrid CF & Ufaransa)
Marcelo (Real Madrid CF & Brazil)
N'Golo Kante (Chelsea FC & Ufaransa)
Luka Modric (Real Madrid CF & Croatia)
Eden Hazard (Chelsea FC & Ubelgiji)
Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain & Ufaransa)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid CF/Juventus & Ureno)
Lionel Messi (FC Barcelona & Argentina)
Messi afunga bao lake la 400 La Liga
Hayo yakijiri, Lionel Messi alifunga bao lake la 400 La Liga na kuwasaidia Barcelona kuwalaza Eibar 3-0 uwanjani Nou Camp, na kurejesha mwanya wa alama tano kileleni.
Sababu ya Ronaldo kuorodheshwa wa 49 duniani
Raia huyo wa Argentina ambaye ndiye mfungaji mabao mengi zaidi katika historia La Liga alifunga bao lake katika mechi yake ya 435.
Messi, ndiye mchezaji wa kwanza kufunga mabao 400 katika moja ya ligi tano za Ulaya, na ndiye mchezaji wa pili kufunga mabao 400 katika mechi za ligi tano kuu Ulaya.
Image caption
Messi alifungia Barcelona bao lao la pili mechi hiyo ambayo walishinda 3-0
Huyo mwingine ni Cristiano Ronaldo ambaye amefunga mabao 409 ligini baada ya kucheza mechi 507, lakini mabao yake ameyafunga England, Uhispania na Italia. Mabao ya Messi yote ni katika La Liga.
De Gea huenda akawa bora zaidi Man Utd - Solskjaer
Bao hilo lake dhidi ya Eibar lina maana kuwa Messi amefikisha magoli 400 mechi 63 mapema kuliko Ronaldo.
Aidha, imefunguza zaidi mwanya kati yake na wafungaji wengine bora katika historia Uhispania, ambapo anafuatwa na Ronaldo mwenye mabao 311 kutoka mechi 292 akiwa Madrid lakini ambaye sasa anachezea Juventus.
Kuna pia Telmo Zarra, ambaye amefunga mabao 251 La Liga ambaye ndiye anayeshikilia nafasi ya tatu
0 COMMENTS:
Post a Comment