TETESI KUBWA ZA MOTO KATIKA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMATATU
Bournemouth iko radhi kumuuza mshambuliaji wa England Callum Wilson kwa Chelsea kwa pauni £75m - mara 25 zaidi ya kiwango walicholipa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mnamo 2014. (Star)
Wolves watapambana na Chelsea katika kuwania kumsajili Wilson, ambaye amefunga mabao 10 kufikia sasa msimu huu.(Birmingham Mail)
Chelsea pia inataka kumsajili upya beki wa kati wa Bournemouth Nathan Ake, miaka miwili tu baada ya kumuuza Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa Cherries. (Sun)
Mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Uhipania Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 33, analengwa na Barcelona. (Mundo Deportivo)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema klabu hiyo haitofikiwa kiwango kinachohitajika kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves mwenye umri wa miaka 21 cha thamani kwa thamani ya £100m (Mirror)
Mshambuliaji wa Watford raia wa Ufaransa Abdoulaye Doucoure, aliye na miaka 26, ameiambia televisheni ya Ufaransa kwamba 'ataondoka' Hornets. (Canal Football Club, via Express)
Winga wa West Ham Michail Antonio anasema mchezaji mwenza wa Hammers na mshambuliaji wa Austria Marko Arnautovic, mwenye umri wa miaka 29, anataka kuelekea China. (Sky Sports)
Aliyekuwa winga wa Liverpool Ryan Babel, mwenye umri wa miaka 32, anakaribia uhamisho kwenda Fulham kwa mkopo. Raia huyo wa Uholanzi kwa sasa anaichezea Besiktas. (De Telegraaf)
Liverpool wanamfukuzia winga wa Celtic na Uskotchi James Forrest, aliye na miaka 27. (Scottish Sun)
Lille imejitosa katika kumwania mchezaji wa kiungo cha kati wa West Ham Pedro Obiang, aliye na miaka 26. Raia huyo wa Guinea ya Ikweta pia analengwa na Fiorentina. (RMC Sport)
Bournemouth itampa mkataba mpya mchezaji wa kati David Brooks, aliye na miaka 21, ili kuondosha matumaini kutoka kwa Manchester United na Tottenham. (Sun)
Fulham, Huddersfield na Leeds ni miongoni mwa vilabu vilivyo na hamu ya kumsajili mchezaji wa Columbus Crew na timu ya taifa ya Marekani Gyasi Zardes, aliye na miaka 27. (Teamtalk)
Leeds pia inapanga kumwania winga wa Wales Daniel James, aliye na miaka 21, na winga wa Ecuador Jefferson Montero, mwenye miaka 29, ambao wote wanaichezea timu ya Swansea.(Sun via Wales Online)
Leeds pia inawania kukamilisha usajili wa kipa wa Southampton Fraser Forster, mwenye umri wa miaka 30, kufikia mwishoni mwa wiki (Star)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment