JEMBE JIPYA YANGA KUIBUKIA TAIFA KESHO
Kiungo mpya wa Yanga, Mohammed Issa ‘Banka’, kesho Jumanne anatarajiwa kuibukia Uwanja wa Taifa wakati kikosi hicho kikipambana na Mwadui FC katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Banka alisajiliwa na Yanga katika dirisha kubwa la usajili lakini ameshindwa kuichezea timu hiyo hadi sasa kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa kutokana na kutumia dawa zisizotakiwa michezoni.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, limeeleza kuwa Banka ataibuka katika mechi hiyo ikiwa ni baada ya kuruhusiwa kuanza kujichanganya katika michezo ambapo atakuwa jukwaani kuisoma timu yake ikicheza.
“Unajua awali Banka hakuwa anaruhusiwa hata kuonekana uwanjani kutokana na ile adhabu yake, lakini kwa sasa kidogo mambo yamelegezwa na ameambiwa aanze
0 COMMENTS:
Post a Comment