ZARI AMTAJA MBADALA MPYA WA DIAMOND
Mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ juzi kati alifungukia mwanaume atakayechukua nafasi ya mzazi mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kudai kuwa si mwanaume anayependa mitandao ya kijamii.
Zari alifikia hatua ya kuweka wazi hayo alipoulizwa kama kweli hana mpango wa kuolewa na Diamond na atamuanika lini mwanaume anayempenda ambapo alieleza kuwa mwanaume wake si wa mitandao ya kijamii.
“Mume wangu siyo wa social media, ni mume wangu siyo wetu,” aliandika Zari alipomjibu shabiki mwingine aliyemwambia atafute mwanaume wa kuzeeka naye.
Baada ya majibu hayo Ijumaa Wikienda lilimsikia rafiki mmoja wa Diamond (jina linahifadhiwa) anayeifahamu vizuri familia hiyo akidai kuwa siku nyingi Zari ana mwanaume anayetoka naye kimapenzi lakini hapendi kuweka wazi kwa sababu mwanaume huyo amemzuia.
“Zari siyo kwamba hana mwanaume tangu aachane na Diamond na si kama hapendi kumuonesha, anapenda sana lakini unaambiwa mwanaume huyo hapendi mambo ya mitandao ya kijamii kwani ni mtu mwenye heshima zake,” alisema rafiki huyo wa karibu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.
TUJIKUMBUSHE
Zari ambaye ana watoto watano wawili kati yao amezaa na Diamond baada ya kuachana na Mbongo Fleva huyo amewahi kuhusishwa kimapenzi na mwanaume anayeitwa Brian wa nchini Uganda ambapo mara mbili tofauti alionekana kupiga naye picha za ukaribu lakini mwenyewe alidai kuwa ukaribu wao huo ni wa kikazi tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment