January 14, 2019



KIKOSI cha Mtibwa Sugar leo kimepoteza mchezo wake dhidi ya Mbeya City uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine.

Mchezo huo ambao ulipaswa uchezwe jana ila uliahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha umekamilika kwa Mbeya City kufanikiwa kuvuna pointi tatu nyumbani.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na mshambuliaji , Eliud Ambokile kwa mkwaju wa penalti dakika ya na kumfanya afikishe idadi ya mabao 10 sawa na Said Dilunga wa Ruvu Shooting kwenye msimamo wa wafungaji bongo.

Mtibwa Sugar wanapoteza pointi sita Uwanja wa Sokoine baada ya kuanza kufungwa na Tanzania Prisons hivi karibuni na leo wamepoteza mbele ya Mbeya City.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic