Na Saleh Ally
SIMBA wamefanikiwa kuwashinda Waarabu wa Algeria, wameifunga JS Saoura kwa mabao 3-0 na kuongoza Kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba wanaongoza kundi lao wakifuatiwa na vigogo, Al Ahly ambao walishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya AS Vita maarufu kama Vita Club ya DR Congo.
Msimamo wa Kundi D, unaonyesha ni Simba wenye pointi tatu, Ahly pointi hizo ila wanazidiwa bao moja, halafu Vita na Saoura wanashika mkia.
Ndiyo michuano hiyo hatua ya makundi imeanza. Simba inaweka rekodi ya kuwa timu ya Afrika Mashariki kuongoza kundi na itakuwa na wakati mgumu wa kuendelea kubaki hapo.
Mechi ya pili ni ugenini dhidi ya Vita Club ambayo tayari imejeruhiwa ugenini Misri. Timu hiyo imefungwa ikiwa pungufu baada ya mchezaji mmoja kutolewa kwa kadi nyekundu.
Kama Watanzania lazima tukubaliane, kuzipa moyo timu zetu ni jambo namba moja ni jambo sahihi na hii ni kazi yetu. Lakini tunapaswa kuwapa ukweli wa hali halisi.
Ninaamini Simba watakuwa wanajipanga na wana bahati ya kuwa na viongozi wenye uzoefu na michuano ya kimataifa. Lakini lazima wakumbushwe na kuelezwa kilicho sahihi.
Kwa wale waliobahatika kuiona mechi Ahly wakishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Vita Club ninaamini watanielewa zaidi.
Niliingalia mechi hiyo ikirushwa moja kwa moja na ZBC2. Ilicheza baada ya Simba kuwa wamemaliza kazi yao dhidi ya Saoura. Ninaamini benchi la ufundi la Simba lilipata nafasi ya kushuhudia pia.
Mechi ilionyesha wazi kwamba Ahly na Vita Club ni timu nzuri. Ukiangalia mchezo ule unaona Vita Club tayari walipata tatizo la kuwa pungufu na ndilo lililowamaliza. Lakini isingekuwa hivyo, bila shaka Ahly wangekuwa katika wakati mgumu.
Uchezaji wa Vita Club ulionyesha ni timu yenye watu wakomavu hasa katika michuano hiyo. Nilishangazwa maana kabla ilielezwa kuwa wameuza wachezaji kadhaa.
Ukweli ni kwamba wachezaji wake wanaelewana kwa kiwango cha juu na wanajiamini. Walifanya mashambulizi kadhaa hatari kwenye lango la Ahly ambao walilazimika kufanya kazi ya ziada.
Bila ya ubishi niseme kwamba kwa kiwango cha Saoura, hakiwezi kuwa sawa na Ahly au Vita Club. Maana yake ni hivi, Simba wana mzigo mzito zaidi mbele yao na mechi zao zote mbili zinazofuata ni za ugenini dhidi ya Vita Club halafu Ahly.
Narudia palepale, kwamba Simba wana timu nzuri lakini wanakwenda kukutana na timu nzuri zaidi na zenye uzoefu zaidi.
Tukubali, Saoura hawana uzoefu na uliona hata Simba walipowashambulia sana hawakuwa na mbinu nyingi zinazoonyesha ni wazoefu na wanaweza kupoza mambo kadhaa.
Angalia utaona, hata zile tabia za Kiarabu hazikuwepo kwa asilimia mia. Simba wameitumia nafasi, wamefanya kile kilichotakiwa, safi. Maana tayari wamekusanya pointi tatu kibindoni.
Wakati wakiwa tayari wana mtaji wao kibindoni, tayari mambo sasa ndiyo yanaanza na wajue kazi hata nusu bado.
Unapokutana na timu kama Ahly au Vita Club, mambo yanatakiwa yaende tofauti kabisa. Wao wanajua namna ya kukupa makosa halafu wakuadhibu.
Mfano, uchezaji wa Juuko Murshid. Bila shaka kwa timu kama Ahly au Vita Club angeenda nje mapema sana. Hakuwa makini ukabaji wake ulikuwa unahatarisha “afya” ya Simba katika mechi hiyo.
Hata mwamuzi wa mchezo huo, pia baadaye alilazimika kutumia nidhamu ya mzazi kumbakiza Juuko uwanjani. Sasa ukikutana na timu ambazo wachezaji wake wanamiliki sana mpira, wanauchezea muda mrefu. Basi lazima suala la ukabaji liwe na nidhamu ya juu sana.
Simba wanaweza kuwafunga Ahly na haitakuwa mara ya kwanza. Lakini lazima wawasome sana na kujifunza mengi. Pia wanaweza kufanya hivyo kwa Vita Club, lakini niwatangulizie maneno haya, itakuwa mechi ngumu ambayo lazima wajipange hasa.
Sherehe za kipigo cha Saoura, zimeisha. Sasa waanze hesabu kwa kuwa muda wenyewe ni mchache, wiki moja kabla ya mechi nyingine huku ukicheza mechi nyingine.
Mechi ya Ahly na As Vita licha ya ukweli yakwamba kuwa As Vita ni wazuri kakini kwa kweli kabisa kama tunataka kuzungumza mpira halisi ni Kwamba Ahly bado hawajakaa vizuri kufikia ile Ahly tunayoifamu na makali yake yasiyokuwa na huruma. As Vita wamecheza pungufu kuanzia dakika 35 za kipindi cha kwanza lakini Ahly licha ya kupata dakika takribani 10 kabla ya mapumziko za kusoma pengo liloachwa na mchezaji wa Vita lakini Ahly walirudi uwanjani kutoka mapumziko wakiwa bado hawajui nini cha kufanya. Mechi kama ya juzi uwakute El Ahly hasa ilio kwenye ubora wao wale Mkongo juuzi basi lazima wangepata kadi nyengine nyekundu kutokana na presha. Ahly alifungwa kwenye fainal na watunisia wakaja kuingia kunako hatua ya makundi kwa kusuasua kupitia kwa waithiopoia na baada ya kuona hivyo wenye timu wakaghadhibika kwa kumtimua kocha pamoja na kuleta wachezaji kadhaa wapya ndani ya timu. Kiuhalisia hivi sasa Ahly ina wachezaji mahiri lakini haina timu. Kocha mpya lazima atahitaji muda kusindika mfumo wake utakaoendana na wachezaji wake hasa kama timu itakuwa imefanya mabadiliko mengine mapya ya wachezaji pia lazima watahitaji muda wa kuzoeana. Hayo kwangu mimi ni mapungufu niliyoyaona kwa Ahly kocha mpya,wachezaji wapya ni kama wanajenga timu mpya. Bado Ahly atabakia kuwa Ahly kwa ubora miongoni mwa timu za Africa na hasa katika kundi D ambalo Simba ni mwanafamilia wa kundi hilo ila Ahly wana mapungufu na wanatakiwa kuwa makini tena sana atakapokutana na Simba. Faida kwa Simba ni kwamba tayari ina kocha aliekwisha zoeana na wachezaji kwa mapana na marefu yaani kama mtu na watoto wake. Wachezaji walishamuelewa kocha wao nadhani hata wakiamuangalia machoni kocha wao basi wachezaji walishajua kocha anataka nini. Faida nyengine kwa Simba ni kikosi kilichokaa pamoja kwa muda mrefu. Wakati mwengine ni vizuri kusajili wachezaji wapya wa kuongeza nguvu katikati ya mashindano lakini vile vile itategemea mchezaji huyo mpya kama atakuja kufiti moja kwa moja kwenye mfumo wa timu. Real ya Zidane iliongozwa na fowadi yenye uwezo mkubwa wa kupachika mabao na viungo mahiri na beki fowadi za pembeni zinazopanda na kushuka huku beki yake ya kati isiotabirka iliongozwa na Ramosi. Kilichombeba Zidane sio kuleta wachezaji wapya wa viwango Katikati ya mashindano bali ni muunganiko wa muda kati ya wachezaji kwa wachezaji na kocha wao waliofanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu. Mimi kwa maoni yangu ni kweli kabisa timu ngumu kwa Simba ni As vita na Simba wana kila sababu ya kuzipa uzito wa aina yake mechi zake zidi ya wakongo hao sio kwamba wapo vizuri tu bali wana kocha pia anaeishi ndani ya Simba ambae ni zahera.kitendo chake cha kufanya kazi Tanzania na kuwa rafiki mpenzi wa kocha wa As Vita kunawapa faida wakongo hao zidi ya Simba. Suala la Juuko ametekeleza majukumu yake kwani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Juuko ni kama vile mtoto aliekuwa amesuswa na wazazi wake anaesubiri kutafutiwa wazazi wengine wa kumlea. Hata kabla ya mechi wengi tulijua Juuko hawezi kuwa kwenye ubora wake na ni Simba waliomtengezea mazingira hayo ila hata hizo rafu alizofanya Juuko ameonesha jinsi gani beki wa kati anatakiwa kuwa kwani huwa hawatakiwi kuonesha upendo kwa mshambuliaji pinzani. Mshambuliaji anatakiwa kujitafakari kabla ya kuchukua maamuzi ya kwenda kumtoroka beki,isiwe kirahisi rahisi tu kama beki ya Simba ilivyofanya kule Zambia kwa Nkana . Tunaimani kwakuwa kocha wa Simba anamuhitaji Juuko hivi sasa basi jicho lake litakuwa karibu nae kumsaidia kumuweka sawa ila tuna vijana wawili wa kitanzania ambao ni mabeki wa kati kwanini wameshindwa kumshawishi kocha awaamini muda wote huo jibu tutakuwa tunalo sisi wenyewe watanzania .
ReplyDeletekuhusu juuko tukumbuke ni beki mzoefu katika mechi kubwa za kimataifa hasa kupitia timu ya taifa, pia tuwe na subira kumsubiria beki wetu salim mbonde apone vizuri na arejee mchezoni, kuhusu kundi letu kikubwa ni mbinu za kocha wetu, simba huwa naiona ina balance kipindi kunapokuwa na viungo wengi nafikri ni muda sasa mo ibtahim, hassan dilunga au niyonzima mmojawapo kuingizwa kwenye mfumo na kuendana na mfumo wa washambuliaji wawili tu
Delete