January 22, 2019


Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, amewachana Simba baada ya kufungwa mabao 5-0 dhidi ya AS Vita katika Ligiya Mabingwa Afrika.

Akilimali amesema ni aibu kubwa kwa timu kama Simba kupata aina hiyo ya matokeo akieleza walisema kuwa wana kikosi chenye thamani ya bilioni 1.3.

Mzee huyo ameongeza kwa kusema ni aibu kubwa na fedha kwa taifa la Tanzania kwani wameitangaza vibaya nchi na hawakustahili kufungwa mabao hayo.

Ameenda mbali zaidi na kumshauri Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kuwa apunguze maneno zaidi ya kufanya vitendo.

Ameeleza kwamba Manara amekuwa akilemba mambo mengi lakini mwisho wa siku wanaambulia sifuri hivyo ni vema akapunguza kupamba mambo.

3 COMMENTS:

  1. huoni hata aibu na umri wako huo umeshuhudia vipigo vingapi vya byanga kimataifa achilia mbali vipigo vya simba tano na sita bila inaelekea unapoteza kumbukumbu kalee vitukuu

    ReplyDelete
  2. Simba kufungwa goli tano wala isiwe taabu. Kweli viongozi walizembea kwenye usajili kujiandaa na hatua hii ya makundi hasa ukitilia maanani baadhi ya wadau tuliwaonya Simba kipindi kirefu kuhusiana na As Vita kuwa ndio timu hatari zaidi kwa Simba lakini wahusika inaonekana wanaona watu humu kwenye mitandao huwa tunapiga porojo tu kwa hivyo viongozi hawana muda wa kufuatilia au kutilia maanini ushauri unaotolewa lakini kiukweli huwa ni maoni yalioyofanyiwa tafakuri kubwa zenye mapenzi ya dhati kwa klabu. Sio wadau wote kutoka oversee wanajifanya wanajua bali kuna wanaojua wanachokizungumza kwenye mada husika hasa kutokana na experience ya maisha wanayoendana nayo kila siku.Tofauti moja kubwa ya maisha kati mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea Tanzania ikiwa miongoni mwao ni kule watu wao kutokuwa na nidhamu ya maisha. Na tukizungumza maisha kwa mwanadamu basi kazi ndio kitu cha kwanza kitakachokuwa utambulisho wa maisha ya mtu. Kulikuwa na uzembe wa kikazi na majukumu hadi kupelekea Simba kupigwa kipigo cha aibu ila hata Real au Baercelona au Manchester city wanaweza kupigwa goli tano ni moja kati ya matokeo ya mchezo wa mpira ila Simba hasa viongozi wanatakiwa kuwa wasikivu kusikiliza maoni ya wadau. Kwa mechi ya As Vita Mwinyi Zahera ndie alieiua Simba.

    ReplyDelete
  3. MWINYI ZAHERA KAIUA VIPI SIMBA !! TUELEZEE KWA UFASAHA ZAIDI ILI TUKUELEWE ULIKUA NA MAANA GANI ??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic