Kocha Mkuu wa JS Saoura, Nabil Neghiz ambao ni wapinzani wa Simba, amefunguka kwa kusema anaelewa wapinzani wao walivyopania kupata ushindi lakini amejipanga kuwazuia.
Kocha huyo atakiongoza kikosi chake hicho kilichotua juzi usiku kupambana na Simba kwenye mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mechi baina ya timu hizo itapigwa leo Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Kocha huyo ameliambia Championi Jumamosi kuwa, anaelewa juu ya Simba wanavyotaka matokeo kwenye mechi hiyo lakini wamejiandaa vya kutosha kuwazuia wapinzani wao wasipate ushindi ambapo kwa kupitia baadhi ya mikanda ya video aliyowaona wakicheza, anajua jinsi watakavyokabiliana nao.
“Najua Simba ni timu kubwa hapa Tanzania na wamejiandaa vya kutosha wapate pointi mbele yetu kwa sababu wapo kwao na wanacheza kwenye ardhi yao, najua kwamba wamepania juu ya hilo.
“Sisi tumejiandaa kama ilivyo wao kuwazuia wasipate ushindi hapa, uzuri ni kwamba tumewaona baadhi ya mbinu zao kwa kupitia mikanda ya video ambayo tuliiona mtandaoni.
“Nawajua Simba kwa sababu tulishakutana kule Uturuki tulipoweka kambi na kocha wao, Patrick Aussems ni rafiki yangu, hivyo naona mechi hii itakuwa nzuri na kali,” alisema Neghiz.
0 COMMENTS:
Post a Comment