KIKOSI cha Mtibwa Sugar leo kitakuwa Uwanjani kumenyana na Mbeya City ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa 21, huku makocha wakitambiana kuibuka na ushindi.
Mchezo huo ilibidi uchezwe jana uliahirishwa kutokana na mvua kunyesha na kufanya Uwanja wa Sokoine kujaa maji.
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema vijana wake wapo tayari kwa mchezo wa leo na watapambana kupata matokeo chanya.
"Kila kitu kipo sawa ni wakati tu kwa wachezaji kufanya kile ambacho nimewafundisha, nina imani mchezo utakuwa mgumu ila tunahitaji ushindi," alisema.
Naye Kocha wa Mbeya City, Ramadhani Nsanzurwimo alisema kuwa ushindani ni mkubwa na lengo lao ni kuweza kupata matokeo chanya.
"Hakuna mwalimu ambaye anahitaji kupoteza, hesabu kubwa ni kupata matokeo, tutapambana kutimiza malengo," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment