MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wametumia dakika 270 Uwanjani kucheza michezo ya kiushindani kwa nyakati tofauti na sehemu tofauti.
Simba wameweka rekodi hiyo kutokana na kushiriki michuano miwili tofauti ambayo ni kombe la Mapinduzi na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Dakika hizo 270 Simba walianza kutumia hivi: siku ya Ijumaa dakika 90 walicheza dhidi ya Malindi hatua ya nusu fainali kwenye kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan wakashinda kwa penalti 3-1.
Pia Jumamosi walitumia dakika 90 Uwanja wa Taifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria walishinda mabao 3-0.
Jana Jumapili walitumia dakika 90 mchezo wa fainali ya Mapinduzi Uwanja wa Gombani Pemba walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Azam FC na kufanya waweke rekodi ya kucheza siku tatu sawa na dakika 270 kwenye mashindano na kutumia viwanja vitatu tofauti.
Kwa kweli ratiba iliwabana lakini wameonesha ujasiri mkubwa. Kutoka kujitoa kuyaenzi mapinduzi ya ZANZIBAR mpaka kwenda kuweka heshima ya nchi katika mashindano ya kimataifa. Wakati Js Soura wanajiandaa kuja kucheza na Simba kocha wao labda kwa kuwa ni Mzawa aliwaomba na kuwasihi wachezaji wake kuzingatia kitu kimoja muhimu zaidi ambacho ni kupambana ili kuipigania Algeria kwa kuwa wao ni wawakilishi wa nchi. Sasa utaona kwa jinsi gani wenzetu wanavyoutanguliza utaifa mbele. Watanzania bado tunamatatizo makubwa ya kujitambua na kuamka na kufahamu yakwamba huu ni wakati wetu wa ushindi katika nyanja mabali mbali. Kama alivyokatishwa tamaa na kubezwa kwa Magufuli hakuna atakachokiweza kukifanya katika masuala ya kuleta maendeleo ya nchi na ndio kampeni zilezile za kuikatisha tamaa Simba zianazoendeshwa na baadhi ya watanzania wanaojifanya au kujiita wachambuzi mahiri wa mpira nchini kama vile ushiriki Simba kwenye klabu bingwa Africa wamefika pale kibahati bahati na tunachopaswa watanzania ni kuweka matarajio makubwa zaidi ya kuiona Simba ikifanya vibaya katika mashindano hayo na tuwache kabisa kuisapoti au kutarajia kuwa Simba inaweza kufanya lolote lile la maana, kwa kweli ni watu na vitu vya hovyo kabisa kuwa nao katika jamii ya kitanzania. kama mtu kashindwa kutoa maoni ya kuihamasisha simba kuwa hakuna kisichowezekana wakimueka Mungu mbele kama watajitoa na kuzingatia nizamu ya mchezo kwani Simba wana Mualimu wa daraja la juu na wanawachezaji wasiokuwa na majina Africa lakini kunako uhai baada ya ushiriki wao huu kumalizika basi lazima wataacha Alama za kukumbukwa barani Africa. Ushiriki wa Simba kufanya vizuri una faida kubwa sana kwa timu yetuya Taifa Kila Simba inapopata ushiriki katika ngazi za Africa ndipo wachezaji wa Simba wanapozidi kukua kiuzowefu na kujiamini zaidi katika mashindano makubwa na ndio maana utaona mechi ya Js Soura Simba wameonekana kujiamini zaidi kuliko mechi ya Nkana na tunaimani mechi inayokuja zidi As Vita wachezaji watakuwa na hali ya kujiamini zaidi katika kupambana na hivyo ndivyo itakavyopelekea Tanzania kuwa na wachezaji wenye viwango vya juu katika mashindano ya kiafrika ni kama vile tunaiandaa Taifa Stars ya Afcon kupitia ndani ya Simba cha msingi watanzania na Tanzania ni kuisapoti Simba na kuwakomalia wachezaji wazawa wasiwe watazamji tu ndani ya Simba lazima wapambane wawe wanapata nafasi ya kucheza ili wapate uzoefu utakaokuja kuibeba Taifa Stars. Waache kuwasikiliza wachambuzi wapumbavu wanaotuaminisha kuwa hatuwezi. Tanzania na Simba tunaweza ila wachezaji wazawa lazima wawe majasiri kuliko wageni wa kuipigania Simba. Kuhusu mechi ya Simba na As Vita ugenini hiyo ni mechi ya jihadi kwa Simba kama kweli tunataka kutinga hatua ya robo fainali. Tumesoma makosa yetu zidi ya Nkana FC ugenini nadhani tumenifunza kitu fulani kutoka kwao. Simba tunahitaji point za ugenini miongini mwa moja ya michezo mitatu ya ugenini ili kujidhatiti zaidi. As Vita ni timu imara na ngumu hasa wakiwa kwao ila kuna kila sababu kwa Simba ya kushinda mechi hiyo ya As Vita ugenini ni mechi ya Fainali kwani mechi inayofuata baada ya As Vita ni Ahly na tuna mechi mbili ugenini kwenye ardhi ya warabu fitna zao za huko hatuhitaji kuambiwa.Kumpiga As Vita ni kitu kinachowezekana ni kujipnga tu and yes we can. .
ReplyDeleteSimba siku zote watafanikiwa tu unashangaa kuna timu zinaitwa za wananchi na inashiriki kimataifa na haifanyi lolote hivi sisi shabiki lialia wa simba wandengeleko sio wananchi?
ReplyDelete