January 12, 2019


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa timu ya Simba anawanyanyua mashabiki wa Simba kwa kuwafanya Simba wapate mabao 2-0 dhidi ya JS Saoura katika Uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Dakika ya 45 Okwi alifanikiwa kutumia uwezo wake wa mguu wa kushoto kumalizia pasi ya Clyetous Chama ambaye alipiga pasi mpenyezo iliyomkuta Okwi akawaminya mabeki waarabu na kumalizia kwa shuti kali.

Dakika ya 52 Okwi anamtengenezea pasi Kagere ambaye anaandika bao la pili kwa Simba.

Dakika ya 67 Kagere anamalizia pasi ya Okwi na kuandika bao la tatu kwa Simba Uwanja wa Taifa.

Mbelgiji anafanya mabadiliko ya dakika ya 86 Okwi anatoka anaingia Shiza Kichuya.

Kwa sasa mpira ni kipindi cha pili huku kila timu ikiwa imepania kupata matokeo, katika harakati za kipindi cha kwanza nahodha John Bocco alipata majeraha akatoka nafasi yake ikachukuliwa na Meddie Kagere.

15 COMMENTS:

  1. Salehe Jembe tafadhali endapo asubuhi kitendo cha Yanga kufanya zoezi mmeandika na kuweka kichwa cha habari Eti "Yanga imepeleka maumivi Simba". Basi andikeni sasa " Simba imepeleka maumivu Yanga" Wamefunga ...na hawajapaki Basi!

    ReplyDelete
  2. Mmeona eeh ndio kila Siku mnatuanfikia Eti Makambo ana mzidi Okwi

    ReplyDelete
  3. Andikeni "Jezi ya Njano Imewaponza JS Saoura!

    ReplyDelete
  4. Sasa Nanyie c Mfungue Website Zenu Muandike Mnavyotaka!!
    Kwann Mashabiki wa Simba Mnapenda Kujifanya Wajuaji Sana Na Kumpangia Kazi Mwandishi Nguli Kama Huyu Na Hata Shafih Dauda Pia.
    Once a Mbumbumbu Always a Mbimbumbu Hahahah

    ReplyDelete
  5. Nadhani mmeelewa maana ya kutuma maumivu..Tumieni busara waandishi hivi timu kufanya mazoezi ya nguvu na kocha kusema watashinda mechi...Basi hivyo vitu viwili vitapeleka maumivu timu nyingine...kweli mwandishi unakaa kwenye kompyuta na kuandika hilo

    ReplyDelete
  6. Jaman mtupe update za injury ya kapombe

    ReplyDelete
  7. This is simba brother
    Yeeeeeees, we can

    ReplyDelete
  8. Nashukuru Niliwatakia Ushindi Mzuri Watani Na Nikweli Mmewakilisha Vyema Nchi Yetu Hongereni Sana

    ReplyDelete
  9. Watu wasipate kigugumizi cha kuipongeza Simba kwa ushindi hata kidogo kwani wakimomaa na tabia hiyo kwa Simba hii wataishia kuwa mabubu. Kuna wanaojiita waandishi wa habari lakini hata kuandika ushindi wa Simba kwa wakati imekuwa nongwa.Isipokuwa nina uhakika kama Simba wangefungwa wangekuwa wa Kwanza kuchapisha habari hizo. Hii inatuonesha jinsi gani watanzania tulivyo watu qa hovyo.

    ReplyDelete
  10. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  11. Muhenga ndo uyo anawakimbiza vjana noma sana okwi tufurahishe wanamsimbaz

    ReplyDelete
  12. Okwiiiiiiiiiiii nani kasema okwi mzeee !!!!!!!

    ReplyDelete
  13. Hivi mliona beki wa Sourra akitambaa baada ya kupigwa chenga na Okwi kwenye goli la kwanza?
    Waandishi wenye roho za
    kwanini mtalazimishwa kukubali.
    Hata kocha wa Sourra kawalalamikia. Badilikeni wacheni roho mbaya. Kuweni na weledi.

    ReplyDelete
  14. Wakilewa sifa baaaas tembo watalitia maji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic