NAHODHA wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, John Bocco amesema mwitikio wa mashabiki Uwanjani umewapa morali kubwa hali iliyowafanya wapate nguvu na kushinda mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura.
Simba walikuwa wakiiwakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa kundi D.
Bocco amesema mashabiki wanaumuhimu na nguvu kubwa wakiwa Uwanjani anafurahi kuwaona namna wanavyokuwa begakwabega na timu yao.
"Tunachoangalia sisi ni pointi tatu bila kujali nani anafunga na nani anakosa, makosa yapo na kwenye mpira mengi yanatokea ila sapoti ya mashabiki inatupa nguvu ya kupambana," alisema Bocco.
Katika mchezo wa leo Bocco alishindwa kumaliza dakika 90 kwani alitoka kipindi cha kwanza baada ya kuumia na na nafasi yake ilichukuliwa na Medie Kagere dakika ya 37.
Mashabiki wa Yanga mnaidhalilisha nchi kushangilia wageni ni mara mia bora mkaae nyumbani kuliko kuja uwanjani na kushangilia mwishoni aibu inawakuta Simba itashinda tu....huu ni mkakati (TFF, Simba wanachama, wageni, Serikali kuu, serikali ya mkoa na Jeshi la Polisi na wadhamini au wawekezaji wa klabu ya Simba) pointi 9....kwa mchina lazima....nguvu moja....ni kauli mbiu kwa vitendo....
ReplyDelete