January 22, 2019


Mkurugenzi wa uendeshaji SportPesa nchini, Abbas Tarimba, amevitaka vilabu vya Simba na Yanga kutumia vikosi vya kwanza ili kuepusha aibu.

Tarimba amesema Tanzania imekuwa ikipatwa na aibu kila mwaka kutokana na kombe hilo kuelekea Kenya kila siku.

Akiongea kwa msisitizo, Tarimba amezitaka timu zote za Tanzania kwa ujumla kuhakikisha zinakuwa siriazi na mashindano hayo ambayo bingwa wake atapa nafasi ya kucheza na Everton.

"Imekuwa ni utamaduni wetu kudharau haya mashindano, awamu hii hatutaki utani, tunataka kombe libaki nyumbani kwa maana kila siku limekuwa likienda nchi jirani. Tunavitaka vilabu vyote vya hapa nyumbani kuhakikisha vinafanya vizuri" alisema.

Ratiba ya michuano hiyo inaonesha kuwa Yanga itaanza kutupa karata yake ya kwanza leo dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya huku Simba wakicheza na AFC Leopards kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic