MZEE AKILIMALI AUWASHA MOTO YANGA, AJA NA KAULI YA KIBABE 'MRUDISHENI HARAKA!!"
Kufuatia kikosi cha klabu ya Yanga kufungwa bao 1-0 na Stand United katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara huko Shinyanga, Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, ameutaka uongozi kumrejesha haraka Beno Kakolanya.
Akilimali ameibuka tena akieleza ana wasiwasi kama Yanga itafanya vizuri msimu huu kutokana na kipa huyo kuondolewa akiamini ndiye nguzo stahiki katika lango la Yanga.
Mzee huyo ameeleza wasiwasi wake kuwa hana uhakika kama timu itafanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kumtegemea Klaus Kindoki, Ibrahim Hamid na Ramadhan Kabwili kwenye lango.
Ameeleza anamwamini zaidi Kakolanya kuwa ni imara anapokuwa langoni na akisema anashangaa kwanini mpaka sasa hajarejeshwa kikosini.
"Nina wasiwasi na Yanga kuchukua ubingwa msimu huu kwani katika nafasi ya lango mpaka sasa Kakolanya hayupo, nautaka uongozi umrejeshe haraka sana ili atusaidie kufanya vizuri" amesema.
Ikumbukwe Kakolanya aliondolewa na Kocha Mkuu wa timu, Mwinyi Zahera kufuatia kugomea kusafiri na timu kwasababu ya madai ya fedha zake za usajili na mshahara.
Asaidie kulipa mishahara ya wachezaji kabla ya kupanua domo lake kwenye media
ReplyDeleteBado Vyura ngojea mpigwe kwenye Sports Pesa mtampigia magoti Kakolanya.
ReplyDeleteKwa hili lazima Kakolanya pamoja na yote anatakiwa kumsamehe kwani Yanga hakuna kipa pale, hata Zahera alitukosea kutuletea kipa mbovu na tulishamsamehe kwa nini yeye asimsamehe Kakolanya?????
ReplyDeleteHuyo mzee njaa tu inamsumbua...
ReplyDeleteKocha wetu anasisitiza NIDHAMU KWANZA. Wachezaji wote sawa na peyote anaweza kucheza na muleta ushindi. Hiyo ndiyo filosofi ya kocha na kweli kwa mechi zote hatutegemei mchezaji mmoja mmoja. Wale walimshawishi kakolanya kuondoka kambini usikuusiku sasa wamtafutie timu ya kucheza. Zahera hana jina la kakolanya kwenye wachezaji wake.
ReplyDeleteMzee akiliman mchango wako mwenyw time mini maana Lila sikujua matamko ya kupinga tu
ReplyDeleteAsiporudishwa vyura wataharisha .Ngoja vipigo vianze .
ReplyDeleteKakolanya ni kipa mzuri ndio lakini pia kocha zahera ni kocha mzuri ndio;sasa najiuliza je kakolanya naye ni mwanadamu anaependa kuishi?, na ni mtu anaetegemewa na familia na jamii inayomzunguka sasa je, angeishi vip kama hapati stahiki zake? nidhamu ni kitu cha msingi sana kwenye soka lakini huyo zahera tayari anapiga kelele yeye anavyanzo vingine vya kuingiza kipato na hawa wachezaji wetu wanategemea mpira jamii yake na familia na mambo mengine yaweze kwenda sasa itakuwaje tumlaumu kakolanya na huku fedha zipo lakini wapigaji ndo wengi Yanga? jamani maisha ya sasa bila fedha hayaendi ukweli kabisa, Zahera anataka kazi yake iende lakini wachezaji nao wanataka familia zao ziishi, lakini alipopata si aliludi kwenye kikosi? sasa kosa lake liko wapi? au mlitaka acheze akiwa na mapenzi na club na si maslahi? kwa sasa hicho hakipo ndugu zangu mpira ni pesa na si maneno maptupu
ReplyDeleteHebu tujiulize kwanza kabla ya Kakolanya kurudi.
ReplyDelete1. Je wanaocheza huku wakidai mishahara kuna mpango gani wa wao kulipwa?
2. Je mshahara ukikosekana tena Kakolanya hatoikimbia timu ama kugoma wakati anategemewa?
3. Je akiikimbia timu wakati anahitajika kutokana na ukata nini kifanyike?
4. Je mnakumbuka wakati Elisha John aliposajiliwa Yanga kutoka Coastal Union nini kilitokea? Ama mmejisahaulisha?
Soka linahitaji nidhamu kwanza sio taarabu