Tshishimbi ambaye alisafiri kwao kwenda kutatua matatizo kadhaa ya kifamilia kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwa mabosi wake, amerejea na leo amehusika katik mazoezini ya asubuhi.
Kiungo huyo fundi bado hajaonesha cheche zake msimu huu baada ya miezi kadhaa nyuma kuwa sehemu ya wachezaji walio majeruhi Yanga.
Hivi sasa kikosi kipo katika maandalizi ya SportPesa Super CUP ambayo itafanyika hapa nchini.
Tayari Tshishimbi ameshaungana na wenzake kambini na kuna uwezekano mkubwa akawa mmoja wa watakocheza mashindano hayo ambayo yanakuwa chini ya udhamini wa kampuni hiyo ya bahati nasibu.
0 COMMENTS:
Post a Comment