UONGOZI wa Singida United umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho wa michuano ya SportPesa Cup dhidi ya timu ya Bandari utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Singida United wataanza kumenyana majira ya saa nane kamili mchana dhidi ya wapinzani wao kutoka Kenya wakitamba uzoefu wao wa kushiriki michuano hiyo utawabeba.
Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema huo utakuwa ni mtihani mwingine kwa benchi lao la ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu, Dragan Popadic ili kuwatoa kimasomaso mashabiki wa Singida United.
"Tumejipanga kuhakikisha kesho tunapata ushindi dhidi ya Bandari ya Kenya, tuna uzoefu wa kutosha katika mashindano haya sasa ni mwaka wa tatu tukiwa tunaishia robo fainali.
"Mwaka huu tupo nyumbani, hivyo ushindi ni lazima chini ya kocha Popadic mwenye cv nzuri na uzoefu wa kutosha, hivyo watanzania hasa wana Dar es salaam waje kwa wingi kuona Singida United inavyo peperusha vyema bendera ya Tanzania," alisema Katemana.
Baada ya Singida kumaliza kumenyana na Bandari majira ya saa 10:00 jioni timu ya Yanga itashuka nayo Uwanjani hapo kumenyana na KK Sharks ya Kenya na kiingilio cha chini ni shilingi elfu mbili tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment