Kocha Mkuu wa Yanga, Minyi Zahera, amefunguka juu ya mataji anayoyahitaji msimu huu wa 2019.
Zahera ambaye amekuwa ndiye mteka habari mkubwa hivi karibuni katika klabu hiyo, ameeleza malengo yake ni kushinda mataji hayo ikiwemo lile la Simba.
Kocha Zahera ameyataja mataji hayo kuwa ni la Ligi Kuu Bara ambalo msimu uliopita lilichukuliwa na Simba.
Aidha, Mkongomani huyo amelitaja Kombe la SportPesa ambalo linatarajia kuanza Januari 22 ya kesho na kulibeba pia lile la FA ili kujiwekea heshima.
Licha ya Yanga kupitia kipindi kigumu hivi sasa anaamini kuwa kikosi chake kitazidi kuwashangaza wengi.
Hakuna kombe la yanga mwaka huu
ReplyDeleteWanahabari ndio mnaotupotosha sana mm nikisikia kwamba yanga wanapitia kipidi kigumu nakereka sana hvi ukitaja club yenye wanachama wengi nchini ni club gani jibu ni yanga, sasa club yenye ufadhili wa maana kwa nchi hii ni yanga, club yenye vyanzo vingi vya mapato ni yanga, club iliyojikusnyia pesa nyingi misimu mitatu iliyoisha ni yanga, sasa mnatupotosha sana nyie wanahabari msitudanganye kwamba yanga inawakati mgumu hata huyu kocha anaetoa pesa kuwapa wachezaji angalieni hzo pesa na tafakarini wale waliomleta zahera haohao ndio waliopiga pesa na sasa wanazitumia ili kuweka mambo vizuri kwa kocha kwa kumpatia ili aweze kulinda heshiam yake ndan ya club wakizid kuzipiga, Mnamuona zahera kwamba ni msemaji mzuri sana lakini kuna mambo ya kusema hilo hawezi kulisema kwani yeye hana familia nae anajua yanga anapita tu sasa kwann asitengeneze mazingira? Ninatambua uendeshaji wetu ni wa figisu figisu subirieni akifanya vibaya mtaona mambo yatakavyokuwa wazi, Lakini yanga ni club tajiri Tanzania ila wapigaji ndo wengi hao wazee wenu wanawatoto wanasoma nje sasa wao watafanyaje? Mazuri yote yanaitaji kuigwa sasa andaeni mazingira ya leo mkasahau ya kesho kwa vyombo vya habari kwamba yanga ni omba omba tu na da nga nywa ndugu zangu haya tuendelea kuona huu mziki bila maamuzi magumu je kesho itakuwaje?
ReplyDeleteMmesikia huko Sportpesa!Jana na juzi Simba walikuwa wanaiaambiwa wametia aibu Taifa..As vita ni ya pili katika msimamo wa ligi DRC.. Na KK Sharks wanashika nafasi ya tano huko Kenya
ReplyDelete