Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa amepata pigo la kuondokewa na baba yake mdogo ambaye amefariki leo Jumamosi huku chanzo cha kifo hicho kikiwa hakijaelezwa.
Kupitia akaunti yake ya instagram, Ngasa ameandika ujumbe unaosema “Pumzika kwa amani baba yangu mcheshi wangu mtani wangu leo hii umetutoka baba R.I.P”
Wakati Ngassa akipata pigo hilo, jana mlimda mlango wa timu hiyo Klaus Kindoki naye Baba yake Mzee Kindoki Nkinzi alifariki na leo anaanza kuitumikia timu yake hiyo, atakwenda msibani baada ya mchezo wa leo dhidi ya Stand United.
0 COMMENTS:
Post a Comment