Nyota wa zamani wa klabu ya Simba Musa Hassan Mgosi ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa timu ya vijana ya Simba, amewatahadharisha wapinzani wao Azam kuwa wanatakiwa kujitathimini juu ya kikosi chao kama kinaweza kumudu uwingi wa mashindano yaliyopo mbele yao baada ya kutumia wachezaji wa kikosi cha kwanza kwenye kombe la mapinduzi.
Azam ndio mabingwa wa kombe hilo kwa mara ya tatu na wametumia kikosi chao cha kwanza katika mechi zao zote tofauti na wenzao Yanga na Simba ambao walipeleka vikosi B kwa ajili ya kuwapumzisha wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya ligi kuu.
0 COMMENTS:
Post a Comment