January 12, 2019


KOCHA Mkuu wa JS Saoure ya Algeria, Nabil Neghiz amesema kilichowaponza wakashindwa kuibuka na ushindi mbele ya Simba ni ugeni wa mashindano ya kimataifa.

Neghiz alikuwa Uwanja wa Taifa akiiwaongoza waarabu hao wakiwa na mytanzania Thomas Ulimwengu kutafuta ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kimataifa ambao wamekubali kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0.

Neghiz amesema, Simba sio timu ya kubeza na alikuwa anatambua hilo awali hali iliyomfanya awape mbinu wachezaji wake ila bahati haikuwa upande wake kutokana na maamuzi pamoja na ugeni wao wakapoteza.

"Naitambua Simba ni timu ngumu, ina wachezaji wenye uzoefu na mashindano ya kimataifa tofauti na timu yangu, ila licha ya ubora wao tumeonyesha nasi tunaweza hivyo ni wakati wao kujitahidi kuwa bora zaidi.

"Katika namna nyingine mwamuzi aliwabeba Simba kwani bao la pili halikuwa sawa ila ndo imetokea tumepoteza tuna nafasi ya kujipanga na tumeonyesha kwamba sisi sio timu dhaifu," alisema.

6 COMMENTS:

  1. Kwa Simba hii siwezi kuwalaumu El ahly hata wakienda kusajili Harry Keane wa Spur. Algeria wapo juu kisoka si wa kunyanyaswa vile na Simba lazima Simba itakuwa imepandisha level yake sio wa kubezwa jamani ni wa kuchukuliwa serious.

    ReplyDelete
  2. Simba wanaweza hilo haling ubishi. Sasa timu eindelle na mazoezi. Iongeze UMAKINI wa kulenga goli, UMAKINI wa kulinda , iongeze SPIDI ya kucheza kwenda golini kwa timu pinzani, iendelee kuheshimu wapinzani na kuendelea kuweka nidhamu ya mchezo. SIMBA moto.

    ReplyDelete
  3. kama mliitazama vizuri mechi ya jana kati ya Al Ahly na Vita itabidi mpunguze hizo tambo msubiri mechi zijazo maana hii timu mliyocheza nayo bado changa sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. hee hiyo timu ya Algeria imeshakuwa under dog? mpira ni dk 90

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic