KOCHA wa timu ya Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa wamejipanga kubeba pointi tatu mbele ya African Lyon katika mchezo wao wa leo utakaochezwa Uwanja wa Manungu.
Mtibwa wanaingia Uwanjani leo wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha suluhu kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Ndanda huku African Lyon nao wanaingia wakikumbuka kupoteza mbele ya Singida United.
Katwila amesema kuwa anatambua upungufu mkubwa wa kikosi chake ni sehemu ya ushambuliaji hali ambayo imemlazimu kufanyia kazi kwa ukaribu.
"Michezo yangu mingi nimeshindwa kupata matokeo haimaanishi kwamba nina kikosi kibaya hapana, ni mapungufu madogo hasa kwenye safu ya ushambuliaji ambayo nayafanyia kazi.
"Imani yangu ni kuona wachezaji wanaibuka kidedea na kubakiza pointi nyumbani hiyo ndiyo kazi ambayo nimewapa, mashabiki na wapenda soka sapoti zao ni muhimu kwetu," amesema Katwila.
0 COMMENTS:
Post a Comment