February 8, 2019


BAADA ya Ligi ya Wanawake kumalizika mzunguko wa kwanza, Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umewakumbusha wamiliki wa timu kuzingatia muda wa kufanya usajili wa wachezaji wao ikiwa ni pamoja na Simba Queens, Yanga Princess, Mlandizi Queens, Marsh Queens.

Msimu huu kwenye Ligi ya wanawake umezikutanisha pia timu za watani wa jadi, Simba Queens na Yanga Princess ambapo Yanga Princess ilipanda daraja msimu huu.

Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo amesema muda wa usajili uliopangwa ukipita hakutakuwa na muda wa kuongezwa.

"Dirisha la usajili limefunguliwa Februari 4 mpaka 25 Februari muda hautaongezwa kwa wale ambao watachelewa kufanya usajili kwani hakutakuwa na salia mtume, na mfumo unaotumika ni wa TFF Connect," amesema Ndimbo.

Ligi ya wanawake inashirikisha timu 12 ambapo mpaka tayari timu zote zilicheza michezo 11 huku kinara akiwa na JKT Queens akiwa amekusanya pointi 33.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic