February 9, 2019


LICHA ya Mwadui FC kufungwa mabao 3-0 na kikosi cha Simba kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Alhamisi, kocha wa Mwadui Ally Bizimingu amesema bado kikosi hakijakomaa kupata matokeo kimataifa hivyo wanapaswa wajipange upya.

Ally Bizimingu amesema kwa namna kikosi cha Simba kilivyocheza kinatakiwa kubadilika haraka kwani wachezaji wake wengi ni wazembe na wanafanya makosa ya kiufundi ambayo ni hatari kwa timu.

"Kwa namna Simba walivyocheza nasi licha ya kushinda bado walikuwa wanafanya makosa ya kiufundi hali itakayowagharimu kwenye michezo yao ya kimataifa.

"Wachezaji wangu walikosa umakini hasa wanapofika eneo la hatari, nadhani kama wangekuwa na uzoefu na makini kwa nafasi ambazo tumetengeneza tungewafunga mabao zaidi ya manne, hivyo kikosi kinapaswa kibadilike," amesema Bizimingu.

Simba jumanne watakuwa na mchezo wa kimataifa hatua ya makundi ambao utakuwa wa marudiano dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic