February 10, 2019


MSHAMBULIAJI wa zamani wa kikosi cha Yanga, Mohamed Hussen 'Chinga' amewapa somo wachezaji wa Simba ili wafanikiwe kumyoosha Mwarabu Jumanne kwenye mchezo wa marudiano hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa.

Simba inaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa na itacheza na Al Ahly ya Misri Jumanne Uwanja wa Taifa ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza walipokuwa ugenini.

Chinga amesema wachezaji wa Simba wanashindwa kupata matokeo kutokana na uzembe wawapo uwanjani kwani wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

"Wachezaji wa Simba wanapaswa wajitambue wawapo uwanjani wachezaje kwa ari ya kutafuta ushindi na kushirikiana, endapo watafanikiwa katika hilo watapata matokeo chanya yatakayowapa nafasi ya kusonga mbele.

"Safu ya ushambuliaji inatakiwa iwe makini kumalizia mipira eneo la hatari, pia wachezaji wote kiujumla waache tabia ya kukaba kwa macho inaigharimu timu, ni wakati wao kupeperusha bendera ya Taifa," amesema Chinga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic