BAADA YA KICHAPO CHA JANA, YANGA WAIVAA BODI YA LIGI
Baada ya kupoteza mchezo wa pili katika Ligi Kuu Bara hivi sasa, baadhi ya wanachama wa Yanga wameilalamikia Bodi ya Ligi ya TFF kwa kuchelewesha kutangaza majina ya waamuzi wa mechi ya watani.
Mwanachama anayejulikana kwa jina la Abdallah Chitemo, amesema Bodi ya Ligi inapaswa kumtangaza Mwamuzi walau siku 6 kabla kuelekea mechi hizo.
Wasiwasi wa Chitemo umekuja akieleza yawezekana kukawa na njama zinapangwa ili kuwaharibia Yanga makusudi kutokana na Bodi hiyo la Ligi kuchelewesha utangazaji wa Mwamuzi.
Ameeleza kuwa katika nchini zilizoendelea Mwamuzi hutangazwa mapema zaidi na akiwataka Bodi kujitathmini upya ili kuepuka lawama zisizo na msingi.
Katika mchezo uliopigwa Taifa jana, Yanga ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Simba ambalo lilifungwa na Meddie Kagere kwenye dakika ya 71.
Tatizo msomali yupo pale hakuna kitu kinachoendelea zaid ya polojo tu mamae
ReplyDeleteHayo ni ya yanga kila pale wapochezea kichapo na tuliyajuwa kuwa yatatokea. Yanga inajihisi ni timu isiyofungika na kichapo walichokipata kilitabiriwa tokea mwanzo na kujulikana kuwa watasingizia njama mbaya. Ilitabiriwa kuwa watafungwa kutokana,na uwezo mkubwa wa Simba wa uwanjani na hasa baada ya kuwafunga wale machampioni wa kombe la Afrika Al Ahli na pia uwezo wa hela na sio wakuzungusha bakuli mwendo wa yanga wa kusuwasuwa na baada ya kuingia Manji mitini na sasa yanga wajiweke tayari kupambana na michezo ijayo ambayo itakuwa migumu sana
ReplyDeleteWaamzi Wajana Walikuwa Safi Tu Zaidi Waliibeba Yanga Kwa Hiyo Huyo Mwana Yanga Alita Yanga Ipige Penati Baada Ya Tambwe Kujaribu Kufungia Mkono Manura Akadaka Au Alitaka Refarii Asimpe Tambwe Kadi Kwa Kutumia Mkono Makusudi Kupiga Mpira Wakati Ile Football/Mpira Wa Miguu Au Bodi Ime Husika Wapi Na Mwamzi Kahusika Wapi Au Ndo Tayari Kachanganyikiwa
ReplyDeleteHakika na kweli sasa Yanga mnachanganyikiwa bila sababu!. Mwamuzi kama angetangazwa kama mnavyotaka mngefaidika vipi, au mngeepusha vipi kichapo? au ndo nyinyi huwa mnawatafuta waamuzi kumaliza mchezo nje ya uwanja?. Au uwanjani mwamuzi anakuwaje yaani kwa upande wenu yanga pindi anapotangazwa mapema! Au akitangazwa mapema mnamchukua mnampeleka kwenye kambi yenu Moro kuanzia siku ya kwanza ya kambi hadi ya mwisho nae anawapa mbinu za ufungaji? Maana siwaelewi kabisa concept yenu na utangazaji wa mwamuzi mapema! Msiache kutambua kuwa Ubora wa kikosi na mbinu ndivyo vilivyoamua matokeo ya mechi ya jana. Hayo mengine ni porojo tu za utetezi. Maana jana mmehukumiwa, na siku zote huwezi kutoa hukumu bila ya mhukumiwa kujitetea, hivyo hiyo ni nafasi yenu ya utetezi.
ReplyDeleteHii inaitwa kukosa kisingizio
ReplyDeleteKwa hiyo huyo mwamuzi alimwambia boko atoe assist kwa kagere na kumwambia yondani aikose ili kagere apige kichwa . mmejitakia wenyewe mechi ya kwanza ilikuwa simba vs kakolanya , tukawashauri kwa mechi hii muwapange kabwili na kindoki kwa pamoja mkagoma , mmejitakia wenyewe kufungwa msimlaumu refa
ReplyDelete