February 17, 2019


Wekundu wa Msimbazi Simba SC imewatetemesha watani wao wa jadi Yanga SC kwa kuipa kipigo cha bao 1-0 katika mchezo mkali uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 

Bao pekee la Simba limefungwa na Meddie Kagere dakika ya 71 kwa kichwa akimalizia krosi ya John Bocco na kuamsha shangwe za kutosha kwa mashabiki wa timu hiyo waliofurika ndani ya Dimba la Taifa.  

Katika mchezo huo paulikuwa na matukio mengi ya kimchezo yaliyokuwa kivutio, hapa tumekukusanyia matukio tisa muhimu yaliyojiri kwenye mchezo huo zikiwemo kosakosa za kila upande, jaribio la kutumia mkono kufunga goli lililofanywa na Amissi Tambwe, mbwembwe za Meddie Kagere alipofanyiwa mabadiliko bila kusahau goli lenyewe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic