Beki Zana Coulibally amewashukuru mashabiki wa Simba ambao walionyesha kumuunga mkono wakati akiendelea kurejea katika kiwango chake.
Zana amefanya hivyo mara tu baada ya mechi dhidi ya Yanga na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Meddy Kagere.
Mara tu baada ya mechi, Zana aliwafuata mashabiki wa Simba na kuwaonyesha ishara ya shukurani na baadaye kusema, walimvumilia na sasa ameanza kupata kiwango chake.
Baada ya kutua nchini, Zana alikuwa gumzo akionekana hana kiwango kizuri kama ambavyo wengi walitarajia.
Hata hivyo ilielezwa hakuwa katika kiwango kizuri kwa kuwa hakuwa amecheza kwa muda mrefu.
Kulingana Na Clip Zake Alikua Ktk Kiwango Kikubwa Namimi Nilikuwa Na Imani Naye Nakumbuka Nilibishana Sana Vijiweni Nikimtetea Zana Nahata Nilishawahi Kutoa Comment Nikauliza Wadau Kuhusu Kiwango Cha Zana Kwenye Blog Hii Sasa Majibu Yamepatikana Zana Anatisha Hakuna Tena Uchochoro Kwenye Beki 2 Ya Simba Na Anafanya Vizuri Kwenye Kuanzisha Mashambulizi
ReplyDeleteHakika, Zana ni mchezaji ambaye naamini kwa uchezaji wake wa sasa, hakuwa katika hali nzuri aidha kiutimamu au fitness, nahisi alikosa mechi nyingi za kushindana. Kwasasa anaonyesha anarudi taratibu, ila wakati akiendelea kurudi namshauri azidishe zaidi umakini katika kurudisha mipira nyuma kwa kipa. Maana kuna mpira aliurudisha nyuma kwa Manula siku ya mechi na Ahly, hakika haikutofautiana na ile pasi aliyotuchoma Kesi ambaye kwasasa yupo Nkana siku Simba ilipocheza na Yanga na hatimaye Ngoma kuuchukua mpira kirahisi na kufunga. Zana nae alifanya vile siku tunacheza na Ahly, kilichosaidia ni ushapu wa Manula tu na alikwenda kuukuta mpira nje ya 18. wakati huo forward wa Ahly alikuwa anauwania na alishamuacha Zana.
ReplyDelete