February 16, 2019




Mshambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Okwi na beki kinda wa Yanga, Paulo Godfrey walikuwa kivutio kikubwa leo.

Simba imeshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Yanga ambayo sasa imepoteza mechi yake ya pili katika Ligi Kuu Bara.

Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ilikuwa ni ya vute nikuvute kila upande ukionyesha ulikuwa umepania kushinda kwa kutumia mbinu zake.


Okwi aliyekuwa akicheza wingi ya kushoto, alikutana na Paulo ambaye alikuwa beki wa kulia na ushindani wao, uliwafanya wengi kuwatazama kwa ukaribu.

Mara kadhaa, Paulo alilalamika kutendewa madhambi na Okwi na alikuwa akilipa kwa kumkaba kibabe.

Paulo ambaye amechukua namba hiyo "mkononi" mwa Juma Abdul, wa kiasi kikubwa alifanikiwa Okwi asipeleke madhara.

Mara moja, Okwi alifanikiwa kuachia mkwaju mkali uliopiga mtambaa wa panya na mara kadhaa Okwi naye alilazimika kuwa mbabe dhidi ya beki huyo maarufu kama Boxer kutokana na kasi yake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic