ZAHERA ATUMA KOMBORA JINGINE TENA TFF
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Singida United ya mjini Singida, Kocha Mwinyi Zahera amefunguka tena kuhusiana na ratiba ya ligi.
Zahera ameeleza hakika ratiba imekuwa si rafiki kwao ukiangalia kumekuwa na changamoto ya usafiri kutumia umbali mrefu wakiwa kwenye gari.
Zahera amesema wanapatwa na uchovu kwani tena wanapaswa kurejea Tanga kwa ajili ya mechi dhidi ya JKT Tanzania.
Amewataka Bodi ya Ligi kupitia TFF kuwa wanapaswa kujipanga kwakuwa wachezaji wake wanachoka na wanaweza wasihimili mikimikiki ya ligi kwasababu wanakuwa wanatumia nguvu nyingi.
Katika mchezo huo wa jana, Yanga ililazimishwa suluhu ya bila kufungana na ukiwa na mchezo wake wa pili ikikosa alama mbili baada ya Coastal Union ambayo walienda nayo sare ya 1-1.
Acha kuzingua hivi kweli hukujua sio rahisi kuvuna point uwanja usio wako....mbona alilalamikia ratiba ya awali kabisa ambapo mechi tatu za Yanga ilikuwa ianze nje ya Dar! Ratiba imebana kwa kila timu .
ReplyDeletehatua ni ngumu hasawa kwatimu kama yanga maana watu wa mikoani hukamikia timu kubwa tena ukizingatia hutua hii ya lala salama hivyo yanga wakubaliane matokeo.
ReplyDeleteAcha kelele Zahera, kwani hela za kupandia ndege kwasasa hakuna? kumbe mlikuwa mnajisifu kupanda ndege kwavile mechi zile za Mwadui na Kagera mlishinda? Tafuteni nauli za ndege mkiona wachezaji wanachoka kwenye mabasi. Acha visingizio, Yanga haijaumbwa kushinda tu.
ReplyDeleteKwan timu nyingine wao hawasafiri ? Mbona hawalalamiki?
ReplyDeleteHizi hapa ratiba za Simba na Yanga kwa mwezi huu Februari 2019
ReplyDeleteSIMBA SC
��07/02/2019
Simba vs Mwadui - Dar
��12/02/2019
Simba vs Al Ahly - Dar
��16/02/2019
Yanga vs Simba - Dar
��19/02/2019
Africa Lyon vs Simba - Arusha
��22/02/2019
Azam vs Simba - Dar
��26/02/2019
Lipuli vs Simba - Iringa
��03/03/2019
Stand United vs Simba - Shinyanga
��09/03/2019
Js Saoura vs Simba - Algeria
��16/03/2019
Simba vs As Vita - Dar
��18/03/2019
Simba vs Ruvu Shooting - Dar
��31/03/2019
Simba vs Mbao - Dar
YANGA SC
��06/02/2019
Singida United vs Yanga -Singida
��10/02/2019
JKT Tanzania vs Yanga -Tanga
��16/02/2019
Yanga SC vs Simba -Dar
��20/02/2019
Mbao vs Yanga -Mwanza
��25/02/2019
Namungo vs Yanga -Lindi
��02/03/2019
Alliance School vs Yanga Mwanza
��10/03/2019
Yanga vs KMC -Dar
��16/03/2019
Lipuli FC vs Yanga -Iringa
March 25-30 ASFC robo fainali
HAPO NANI WA KULALAMIKIA RATIBA KATI YA SIMBA NA YANGA??? AFADHALI YANGA INA NAFUU. KAZENI BUTI LIGI HIYO.