UONGOZI wa KMC, umesema utalipiza kisasi cha kupoteza mchezo wao dhidi ya Lipuli kwa mchezo wao wa leo mbele ya Alliance FC ya Mwanza, mchezo utakaochezwa, Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anuary Binde amesema kuwa tunzo ya kocha wao Ettiene Ndiragije kuteuliwa kuwa kocha bora wa mwezi Januari pamoja na mchezaji Dickson Ambudo wa Alliance kuwa mchezji bora kutaongeza ushindani.
"Mchezo wa kwanza tulipoteza mbele yao tulipokuwa ugenini kwa kufungwa mabao 2-1 tulipocheza nao Nyamagana, hivyo leo Uwanja wa Uhuru ni vita.
"Hatutakuwa na beki mwenye kiduku, Ally Aly 'Mwarabu' kwa kuwa ana kadi tatu za njano na Omary Issa ambaye ni majeruhi na ameanza mazoezi mepesi," amesema Binde.
KMC ipo nafasi ya tano baada ya kucheza michezo 24 ikiwa na pointi 35 kibindoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment