BAADA ya Coastal Union kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa nyumbani, Mkwakwani, leo watakuwa ugenini kumenyana na Mbao FC.
Coastal Union watacheza na Mbao wakiwa na mwendelezo wa sare mfululizo nyumbani kwani walianza kugawana pointi na Yanga kisha wakagawana pointi moja na Ruvu Shooting hivyo wanaingia vitani wakiwa na maumivu ya kupoteza pointi nne.
Wapinzani wao Mbao ambao wapo chini ya kocha Ally Bushiri wanangia Uwanjani wakiwa na hasira za kupoteza pointi tatu mkoani Mbeya mbele ya Prisons.
Mbao wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wakiwa na pointi 33 baada ya kucheza michezo 24.
Coastal Union wana pointi 30 wakiwa nafasi ya tisa baada ya kucheza michezo tisa.Hivyo matokeo ya leo kwa kila timu yatakuwa na mabadiliko ya kuipandisha ama kuishusha kwenye nafasi.
0 COMMENTS:
Post a Comment