KOCHA wa timu ya Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa wamejipanga kubeba pointi tatu mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo wao wa leo utakaochezwa Uwanja wa Mwadui Complex.
Mtibwa wanaingia Uwanjani leo wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya African Lyon huku Mwadui FC wanaingia wakikumbuka kupoteza mbele ya Simba.
Katwila amesema anatambua ugumu uliopo kwenye ligi na anapambana kuona kikosi kinakuwa bora hasa kupitia makosa yao.
"Nimeshindwa kupata matokeo chanya kutokana na ushindani uliopo, tupo tayari kuona tunabeba pointi ugenini kujiweka sehemu nzuri zaidi," amesema Katwila.
Mshambuliaji tegemeo wa Mwadui FC, Salimu Aiyee amesema wachezaji wana morali katika mchezo wao wa leo wanasubiri dakika tisini wapate matokeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment