February 11, 2019


POINTI tatu za Mbao FC zinarejea Tanga, bao lililofungwa na Raizin Hafidhi wa Coastal Union iliyo chini ya kocha Juma Mgunda dakika ya 60 kudumu mpaka mwisho wa kipindi cha pili kwenye mchezo uliochezwa leo Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwenye mchezo huo ambao ulikuwa ni wa ushindani dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikamilika kwa timu zote kutofungana.

Beki Adeyum Ahmed wa Coastal Union alipata tatizo la kiafya na kupewa huduma ya kwanza ambayo ilimsaidia akarejea katika hali ya kawaida kwani alibebwa kwa machela.

Mbao wanadondosha pointi sita mfululilizo baada ya kuanza kupoteza mbele ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya na leo wakiwa nyumbana na Coastal Union.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic