February 11, 2019


OFISA Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuelekea katika mchezo wa watani wa jadi ulinzi umeimarishwa na kuwataka mashabiki kuwa watulivu.

Yanga na Simba watamenyana Februari 16 Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

Katika mchezo huo viingilio vimegawanywa katika makundi matatu ambapo kiingilio cha chini zaidi kitakachotoa fursa ya kumuona kinara wa mabao wa Yanga Heritier Makambo na yule wa Simba Meddie Kagere ni shilingi 7,000 (Buku saba) kwa viti vya mzunguko.

Viingilio vingine katika mchezo huo utakaopigwa saa 11:00 jioni vitakuwa ni shilingi 30,000 kwa VIP A na 20,000 kwa VIP B na C.

Mzunguko wa kwanza wa mchezo huu ambao Simba walikuwa ni wenyeji ulikamilika kwa suluhu ya bila kufungana licha ya Simba kufanya mashambulizi mengi ila mlinda mlango Beno Kakolanya alikuwa mbabe wa shoo.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic