UONGOZI wa Coastal Union ya Tanga umesema kuwa kupoteza pointi tatu mbele ya Mwadui FC kumewapa maumivu makali ambayo yanapaswa yalipwe kishujaa.
Coastal Union walikubali kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui mchezo uliochezwa Uwanja wa Mwadui Complex kesho wataikaribisha Azam FC ambayo nayo ilipoteza mbele ya Prisons.
Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda ametuma ujumbe kwa wapinzani wao Azam FCkwa kuwaambia kuwa ushindani uliopo kwenye ligi ni mkubwa wasitarajie wapesi kwao.
"Kupata pointi tatu kanda ya Ziwa ni shughuli zito ila haina maana kwamba hatuna uwezo tupo vizuri, makosa tunayafanyia kazi na tunajipanga upya kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC, tutatumia vema uwanja wetu wa nyumbani," amesema Mgunda.
Coastal Union wanashika nafasi ya saba baada ya kucheza michezo 25 wakiwa wamekusanya pointi 33 kibindoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment