KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema anashangazwa na uwezo wa Amiss Tambwe kushindwa kuibeba timu yake na katika mchezo wao dhidi ya Simba.
Yanga alikuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo ilikubali kulala kwa bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere.
Zahera amesema kuwa kiwango kibovu kilichoonyeshwa na Tambwe kimeiponza timu na kuwafanya wapoteze mchezo wao ambao ulikuwa ni wa ushindani.
"Tambwe ni mchezaji mzuri ila alishindwa kuonyesha uwezo wake wote na alicheza chini ya kiwango, hakuna alichokifanya uwanjani zaidi ya kurukaruka tu.
"Nililazimika nimtoe kipindi cha pili nafasi yake ikachukuliwa na Mrisho Ngassa kutokana na sababu za kiufundi, ila bado tuna kazi kubwa ya kufanya mbele yetu ili kuwa katika ubora," amesema Zahera.
Kashindwa kwasababu kazidiwa nguvu
ReplyDeleteLabda Nayeye Kapewa Rushwa Na Viongozi Wa Timu Tajiri
ReplyDeleteNadhani Tabwe ndo anaishiaishia hivyo kabla ya kutundika ndaruga.
ReplyDeleteUmri mzee, pale analazimisha tu.
ReplyDeletetena mmefungwa bao chache
ReplyDelete