February 21, 2019




Yanga haijafurahishwa na kauli iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ambaye ni shabiki na mwanachana wa kauli hiyo.

Wakati akihojiwa, Muro alisema Kocha Mkonomani wa Yanga, Mwinyi Zahera ni mhamasishaji tu huku akiwaita wachezaji wakongwe wa Yanga, Mrisho Ngassa na mwenzake Haruna Moshi 'Boban', ni wazee.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Lyimo alisema kuwa alikuwa kiongozi wa Yanga alipaswa kutupa ushauri lakini kwa kauli aliyoitoa imewakera na kwa nafasi yake aliyokuwa nayo hakupaswa kuzungumza hayo.

Lyimo alisema, kauli hiyo imemkera zaidi Zahera na kushamngaa mkuu huyo wa wilaya kwa kitendo hicho, lakini viongozi walikaa na kocha na wachezaji hao kwa ajili ya kuzungumza nao kwa ajili ya kuwatengeneza kisaikolojia kabla ya mchezo wao na Mbao FC waliofanikiwa kushinda mabao 2-1.

“Muro ni kiongozi mkubwa serikalini hivi sasa, lakini tunashangaa na hizo kauli zake anazozitoa kwenye vyombo vya habari juu ya kuhusina na wachezaji na kocha wetu Zahera.

“Hatakama wachezaji wetu wazee, sisi ndiyo tuliowasajili na tumefanya hivyo baada ya kuwaona wanahitajika katika timu na uzuri kocha mwenyewe ndiye aliyewahitaji  wasajiliwe," alisema Lyimo.

Hata hivyo, tayari Muro alishaomba radhi kuhusiana na suala hilo akisema waliomkwaza wamsamehe.


2 COMMENTS:

  1. Hao ni Yanga masilahi walikuja hapo wakati wa pesa za manji tu Zahera anafundisha timu ya Taifa ya Congo hivyo hawezi kuwa mbabaishaji

    ReplyDelete
  2. Huyu Muro siyo Yanga Original alifuata hela tu Yanga Enzi za Majini
    , ajiandae Kisaikolojia kugeuzwa Mzungu wa Nne na Manara!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic