February 15, 2019

KESHO Jumamosi, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga itakuwa mwenyeji wa Simbakatika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, miongoni mwa wachezaji nyota waliotumikia timu hiyo kesho wanatarajiwa kuukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa upande wa Yanga, wachezaji wawili hawatakuwa sehemu ya mchezo nao ni mlinda mlango, Beno Kakolanya ambaye hayupo na timu kwa muda mrefu kutokana na matatizo yake na kocha mkuu, Mwinyi Zahera kugoma kumtumia.

Juma Mahadhi anasumbuliwa na majeruhi hivyo hatakuwa sehemu ya mchezo.

Kwa upande wa Simba ni Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi, Shiza Kichuya amejiunga na kikosi cha ENPPI nchini Misri.

3 COMMENTS:

  1. Kichuya sio mchezaji tena wa Simba.

    ReplyDelete
  2. Mwandishi aacha kupotosha watu "unaposema Beno ana matatizo na kocha wake una maanisha nini" kwani usiseme tu kwamba ni yeye ndiye aliyegoma na na kujiondoa kambini akishinikiza kulipwa haki yake ndio aendelee kuitumikia timu pia unasahau kwamba ameomba kuvunja mkataba na yanga badala yake una mtia lawani kocha wa Yanga kuwa muwazi tafadhali acha kuchanganya watu na kuficha maovu ya Beno

    ReplyDelete
  3. Tumia akili kama huna uliza utasaidiwa!Kichuya hayuko Simba tena na Kakolanya alishaachana na Yanga siku nyingi!Tusiandike andike pumba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic