JACKPOTI bonasi ya SportPesa imeongezeka wiki hii ambayo imefikia shilingi 503, 169, 860 kwa wateja watakaofanikiwa kushinda ubashiri wao kwa usahihi kwenye mechi 13.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wa jijini Dar es Salaam, Sabrina Msuya alisema kuwa ili kushinda jackpoti ni lazima uweke ubashiri wa mechi 13 za Jackpoti kwa usahihi na moja kwa moja utajiongezea nafasi ya kushinda.
Msuya alisema, hiyo ni Jackpoti kubwa ya nusu bilioni, awali walianza na shilingi milioni 200 na ikazidi kuongezeka kadri siku zinavyoenda.
Aliongeza kuwa, ni matarajio yao makubwa kuona Watanzania wakishiriki mchezo huo wa kubashiri kutokana na kiasi hicho cha fedha ambacho kinamtajilisha mtu na kubadili maisha yake moja kwa moja.
“Kutokana na hali ngumu ya kimaisha, ninaamini kama Mtanzania atafanikiwa kushinda kiwango hicho cha fedha, basi kitamsaidia kupunguza ugumu wa maisha kwani kupitia kiasi hiki cha pesa atajikwamua na vitu mbalimbali na kujiinua kiuchumi.
Mtumiaji wa mitandao yote ya simu anaweza kucheza na SportPesa kwa kuweka ubashiri wake kwa njia na ujumbe mfupi, ussd pamoja na kwa kupitia website yetu ambayo ni www.sportpesa.co.tz.
“Tofauti na Jackpoti hiyo kubwa, pia tumweka bonasi kwa wale washindi watakaofanikiwa kubashiri mechi 10 hadi 12 kwa usahihi na kushinda kiasi cha fedha ambacho tumeweka na mshindi ana shinda kila wiki,”alisema Msuya.
0 COMMENTS:
Post a Comment