February 15, 2019





Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika kikao chake Februari 9, 2019 chini ya Mwenyekiti wake Wakili Kiomoni Kibamba ilipitia mashauri 15 yaliyowasilishwa mbele yake na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, na kufanya uamuzi ufuatao;


Mmiliki wa Changanyikeni Rangers FC, Omary Bawazir amepewa Onyo Kali kwa mujibu wa Ibara ya 10(a) ya Kanuni za Nidhamu za TFF baada ya kukiri kuingia uwanjani katika eneo la kuchezea (pitch) wakati wa mechi dhidi ya Cosmopolitan iliyochezwa Februari 2, 2019 Uwanja wa Chuo cha Bandari, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Kamati imeshindwa kumtia hatiani kwa kosa la kumpiga Mwamuzi kutokana na Mlalamikaji kushindwa kuthibitisha tukio hio. 

Pia Kamati imekazia faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa Changanyikeni Rangers FC iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72), na kuwa faini hiyo ilipwe ndani ya siku 30.

Katibu Mkuu wa Rhino Rangers, Bw. Dickson Mgalike amefungiwa miezi mitatu na faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kwa mujibu wa Kanuni ya 29(9) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa kuongoza washabiki wa timu yake kuwapiga waamuzi na kamishna baada ya mchezo dhidi ya Arusha United uliofanyika Februari 2, 2019 Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Pia klabu ya Rhino Rangers imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na vurugu hizo. Faini inatakiwa kulipwa ndani ya siku 30 kwa kuzingatia Ibara ya 15(3) ya Kanuni za Nidhamu za TFF.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic