February 15, 2019


WADAU wa maendeleo ya Mpira bongo wamempa ushauri wa bure nahodha wa Simba na mshambuliaji John Bocco ili aweze kubaki kwenye ubora wake aliokuwa nao.

Wadau hao wametoa maoni hayo kupitia Ukurasa wa Saleh Jembe baada ya Uongozi wa Simba kupitia Ofisa Habaari, Haji Manara kuwataka mashabiki wapunguze lawama kwa Bocco kwa kukosa kwake mabao akiwa eneo la hatari.

Mdau wa kwanza amesema "Namuunga mkono Manara, Boko ana mapungufu hayo ya kukosa umakini, na ninakubali kuwa Boko ni bonge la straiker, na pia nakubali kuwa Boko ni mpambanaji. Lakini kama nilivyoweza kumlaumu mara nyingi huko nyuma, anatakiwa kuwa na utulivu na kufikiria zaidi ya kitu kimoja cha kufanya pindi anapokuwa ana kwa ana na golikipa," .

Mdau wa pili amesema "Maana aina ya magoli yote hayo matano (matatu [3] dhidi ya Mwadui, na mawili [2] dhidi ya Al Ahly), aliyakosa kizembe, na yote ni ya namna moja. 


"Anashindwa kufikiria namna nyingine ya kumkwepa kipa pinzani, yeye anachowaza ni kupiga tu, bila kuangalia kipa anakujaje.

Timoth Nkrulu amesema anaungana na Manara kwamba, "Najua siku si nyingi atauonyesha uwezo wake wa kujiamini na kuwa na maamuzi zaidi ya moja na kufuta makosa yake yote hayo".


"Mpira wa kisasa mshambuliaji ana majukumu mengine licha ya kufunga. Anatakiwa asaidie kujilinda, kutoa pasi.


"Mambo ya namba 9 kusimama kuletewa mpira hamna tena.
 Na kama John Boko akishindwa kutimiza jukumu lake hilo ipasavyo basi ajue ana mapungufu ambayo yanaigharimu timu yake kufanikisha malengo yake kwa hivyo ni vyema akajirekebisha na kwa mwanadamu anayejitambua basi ni vizuri kuchukua jitihada za kujirebisha mwenyewe kuliko kuja kurekebishwa," amesema Nkrulu.

5 COMMENTS:

  1. He was good and i do believe he is still good, let us give him time. Tchao

    ReplyDelete
  2. Mbona hii mechi iko wazi sana....kwa uwezo hakuna siri Simba wako vizuri kuliko Yanga kimaandalizi, moral, uwezo wa mchezaji mmoja mmoja....Yanga wanachotegemea ni maajabu ya Soka ambayo yapo....kiukweli Mbona kila kitu kiko wazi sana!

    ReplyDelete
  3. Kweli Bocco Ajirekebishe Atuliage Akiwa Golin Awe Anipiga Shuti Pembeni/karibu Na Mwamba Sehemu Ambazo Goli Kipa Hawezi Kudaka Kwa Urahisi Aepuke Kumlenga Goli kipa

    ReplyDelete
  4. Hivi Bocco hawezi kufinya na kupiga? Siku mojamoja afinye, ampige change kipa na kufunga.sio kuwaza kufumua tuu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli, huo ndo udhaifu mkubwa alionao. Kama utakuwa ndo humjui yaani uwe ndo unamtazama kwa mara ya kwanza, unaweza ukasema labda huyu jamaa ni beki ila leo kapewa tu nafasi ya kujaribu Ustraika. Lakini cha ajabu siku hizi hata mabeki nao wanafinya na wanapiga chenga.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic