BAADA ya Azam FC kupoteza mbele ya Tanzania Prisons ngoma itakuwa hivi:-
Februari 18 itacheza na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Itarejea Dar kumnyana na Simba Februari 22 Uwanja wa Taifa, Dar.
Itafunga mwezi kwa kucheza mechi ya Kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.
Mchezo wa jana unakuwa ni wa pili kwa Azam ya Hans Pluijm kupoteza msimu huu ilianza mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu na Jana Uwanja wa Sokoine.
Kwa matokeo hayo Azam wanaendelea kubaki nafasi ya pili wakiwa wamecheza michezo 23 wakiwa wamekusanya pointi 49.
0 COMMENTS:
Post a Comment